Musa na kichaka kilichowaka moto
1 Basi Musa alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Musa akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu. 2 Huko malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea Musa katika mwali wa moto kutoka kichakani. Musa akaona kwamba ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei. 3 Ndipo Musa akawaza, "Nitageuka sasa nione kitu hiki cha ajabu, nami nione ni kwa nini kichaka hiki hakiteketei."
4 Mwenyezi Mungu alipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, "Musa! Musa!"
Naye Musa akajibu, "Mimi hapa."
5 Mungu akamwambia, "Usikaribie zaidi. Vua viatu vyako, kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu." 6 Kisha akamwambia, "Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo." Musa aliposikia hayo, akafunika uso wake kwa sababu aliogopa kumtazama Mungu.