Pular para o conteúdo
Publicidade

Kutoka 3:1-6

SRUV Swahili Revised Union Version

Mungu amtokea Musa

1 1 Fal 19:8Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu. 2 Mdo 7:30-34;Kum 33:16;Isa 63:9Malaika wa BWANA akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kichaka; akatazama, na kumbe! Kile kichaka kiliwaka moto, nacho kichaka hakikuteketea. 3 Zab 111:2Musa akasema, Nitageuka sasa niende nione kioja hiki, kwa nini kichaka hiki hakiteketei. 4 Kum 33:16BWANA alipoona ya kuwa ameenda ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kichaka, akasema, Musa! Musa! Akaitika, Mimi hapa. 5 Yos 5:15Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni mahali patakatifu. 6 Mwa 28:13;Mk 12:26;Isa 6:1,5;Ufu 1:17Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akafunika uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Basi Musa alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Musa akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu. 2 Huko malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea Musa katika mwali wa moto kutoka kichakani. Musa akaona kwamba ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei. 3 Ndipo Musa akawaza, "Nitageuka sasa nione kitu hiki cha ajabu, nami nione ni kwa nini kichaka hiki hakiteketei."

    4 Mwenyezi Mungu alipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, "Musa! Musa!"

    Naye Musa akajibu, "Mimi hapa."

    5 Mungu akamwambia, "Usikaribie zaidi. Vua viatu vyako, kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu." 6 Kisha akamwambia, "Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo." Musa aliposikia hayo, akafunika uso wake kwa sababu aliogopa kumtazama Mungu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Basi Mose alikuwa anachunga mifugo ya Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani. Mose akapeleka mifugo mbali nyuma ya jangwa, naye akafika Horebu, mlima wa Mungu. 2 Huko malaika wa Bwana akamtokea Mose katika mwali wa moto kutoka kichakani. Mose akaona kwamba ingawa kile kichaka kilikuwa kinawaka moto, kilikuwa hakiteketei. 3 Ndipo Mose akawaza, "Nitageuka sasa nione kitu hiki cha ajabu, nami nione ni kwa nini kichaka hiki hakiteketei."

    4 Bwana alipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, "Mose! Mose!"

    Naye Mose akajibu, "Mimi hapa."

    5 Mungu akamwambia, "Usikaribie zaidi. Vua viatu vyako, kwa maana mahali unaposimama ni patakatifu." 6 Kisha akamwambia, "Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo." Mose aliposikia hayo, akafunika uso wake kwa sababu aliogopa kumtazama Mungu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.