5 Hutaitwa tena Abramu17:5 maana yake Baba aliyetukuka, bali jina lako litakuwa Ibrahimu17:5 maana yake Baba wa wengi, kwa maana nimekufanya baba wa mataifa mengi.
10 Hili ni agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa.
16 Nitambariki, na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki ili awe mama wa mataifa; wafalme wa mataifa watatoka kwake."
17 Ibrahimu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, "Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?"
19 Ndipo Mungu akasema, "Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaka.17:19 maana yake Anacheka Nitalithibitisha agano langu naye kama agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake.
23 Siku hiyo hiyo, Ibrahimu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake, pamoja na wale walionunuliwa kwa fedha zake; kila mwanaume wa nyumbani mwake akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza.