12 Lakini hekima inaweza kupatikana wapi?
Ufahamu unakaa wapi?
13 Mwanadamu hatambui thamani yake;
haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.
20 Ni wapi basi hekima itokako?
Ufahamu hukaa wapi?
21 Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai,
imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.
23 Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima
na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,
28 Naye Mungu akamwambia mwanadamu,
"Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,
nako kujitenga na uovu ndio ufahamu."