Pular para o conteúdo
Publicidade

Ayubu 28:12,13,20,21,23,28

SRUV Swahili Revised Union Version

12 Ayu 11:7,8;Zab 139:6;Mhu 7:24Bali hekima itapatikana wapi?

Na mahali pa ufahamu ni wapi?

13 Mit 3:15Mwanadamu hajui thamani yake,

Wala haionekani katika nchi ya walio hai.

20 Basi hekima yatoka wapi?

Na mahali pa ufahamu ni wapi?

21 Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai,

Na kusitirika na ndege wa angani.

23 Mdo 15:18;Ebr 4:13Mungu ndiye aijuaye njia yake,

Naye anajua mahali pake.

28 Zab 111:10;Mit 1:7;9:10;Kum 29:29;4:6Kisha akamwambia mwanadamu,

Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima,

Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    12 Lakini hekima inaweza kupatikana wapi?

    Ufahamu unakaa wapi?

    13 Mwanadamu hatambui thamani yake;

    haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.

    20 Ni wapi basi hekima itokako?

    Ufahamu hukaa wapi?

    21 Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai,

    imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.

    23 Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima

    na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,

    28 Naye Mungu akamwambia mwanadamu,

    "Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,

    nako kujitenga na uovu ndio ufahamu."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    12 "Lakini hekima inaweza kupatikana wapi?

    Ufahamu unakaa wapi?

    13 Mwanadamu hatambui thamani yake;

    haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.

    20 "Ni wapi basi hekima itokako?

    Ufahamu hukaa wapi?

    21 Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai,

    imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.

    23 Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima

    na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,

    28 Naye Mungu akamwambia mwanadamu,

    ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,

    nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ "

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.