Mwisho: Rafiki zake Ayubu wanafedheheshwa
7 Baada ya Mwenyezi Mungu kusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, "Nina hasira nawe na rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kunihusu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu. 8 Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu atawaombea, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu."