4 Lakini Isa aliposikia hayo, akasema, "Ugonjwa huu hautaleta mauti, bali ni wa kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu." 5 Isa aliwapenda Martha, Mariamu na Lazaro ndugu yao.
15 Hata hivyo nafurahi kwa kuwa sikuwako huko kabla ya Lazaro kufa, ili mpate kuamini. Lakini sasa twendeni kwake."
Isa ndiye ufufuo na uzima
17 Isa alipowasili huko alikuta Lazaro amekuwa kaburini siku nne.
21 Martha akamwambia Isa, "Bwana, kama ungekuwa hapa, ndugu yangu hangekufa.
35 Isa akalia machozi.