16 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni:
"Msisikilize wanachowatabiria manabii,
wanawajaza matumaini ya uongo.
Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe,
hayatoki katika kinywa cha Mwenyezi Mungu.
17 Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi,
‘Mwenyezi Mungu asema: Mtakuwa na amani.’
Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao,
wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’
21 Mimi sikuwatuma manabii hawa,
lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.
Mimi sikusema nao,
lakini wametabiri.