Pular para o conteúdo
Publicidade

Yeremia 23:16,17,21

SRUV Swahili Revised Union Version

16 Mit 19:27;Mt 7:15BWANA wa majeshi asema hivi, Msisikilize maneno ya manabii wakiwatabiria; huwafundisha ubatili; hunena maono ya mioyo yao wenyewe; hayakutoka katika kinywa cha BWANA. 17 Zek 10:2;Mik 3:11Daima huwaambia wao wanaonidharau, BWANA amesema, Mtakuwa na amani; nao humwambia kila mtu aendaye kwa ukaidi wa moyo wake, Hamtapatwa na ubaya wowote. 21 Mimi sikuwatuma manabii hao, lakini walikwenda mbio; sikusema nao, lakini walitabiri.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    16 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni:

    "Msisikilize wanachowatabiria manabii,

    wanawajaza matumaini ya uongo.

    Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe,

    hayatoki katika kinywa cha Mwenyezi Mungu.

    17 Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi,

    ‘Mwenyezi Mungu asema: Mtakuwa na amani.’

    Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao,

    wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’

    21 Mimi sikuwatuma manabii hawa,

    lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.

    Mimi sikusema nao,

    lakini wametabiri.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    16 Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

    "Msisikilize wanachowatabiria manabii,

    wanawajaza matumaini ya uongo.

    Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe,

    hayatoki katika kinywa cha Bwana.

    17 Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi,

    ‘Bwana asema: Mtakuwa na amani.’

    Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao,

    wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’

    21 Mimi sikuwatuma manabii hawa,

    lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.

    Mimi sikusema nao,

    lakini wametabiri.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.