Publicidade

Provérbios 5

3 Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba

hudondoza asali,

na maneno ya kinywa chake

ni laini kuliko mafuta;

4 lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo,

mkali kama upanga ukatao kuwili.

5 Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo;

hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini5:5 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu; kwa Kiebrania ni Sheol..

6 Yeye hafikirii kuhusu njia ya uzima;

njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.

7 Sasa basi wanangu, nisikilizeni;

msiache ninalowaambia.

8 Njia zenu ziwe mbali naye,

msiende karibu na mlango wa nyumba yake,

9 usije ukapoteza heshima yako kwa wengine,

na miaka yako kwa aliye mkatili,

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-