Publicidade

Provérbios 5

8 Njia zenu ziwe mbali naye,

msiende karibu na mlango wa nyumba yake,

9 usije ukapoteza heshima yako kwa wengine,

na miaka yako kwa aliye mkatili,

10 wageni wasije wakasherehekea utajiri wako,

na jitihada yako ikatajirisha

nyumba ya mwanaume mwingine.

11 Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu,

wakati nyama na mwili wako vimechakaa.

12 Utasema, "Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu!

Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!

13 Sikuwatii walimu wangu,

wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.

14 Nimefika ukingoni mwa maangamizi

katika kusanyiko la watu wa Mungu."

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-