1 2 The 2:9Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 Yer 28:9;Mt 7:22ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 Mt 24:24;1 Kor 11:19;2 The 2:11;Ufu 13:14wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda BWANA, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4 2 Fal 23:3;2 Nya 34:31;1 Yoh 1:7;2 Yoh 1:6Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
Publicidade