Maagizo kuhusu fungu la kumi
22 Law 27:30-33;Hes 18:21;Kum 12:6,17;Neh 10:37Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika mavuno yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
29 Kum 10:18;Zab 94:6;Isa 1:17;Eze 22:7,29;Lk 14:12;Ebr 13:2;Kum 15:10;Zab 41:1;Mit 11:24;19:17;Isa 58:7-12;Mal 3:10;Lk 11:41;2 Kor 9:6-11na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.