1 Kut 7:4,14;Kum 2:20;Yn 12:40;Rum 9:18BWANA akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao; kwa kuwa mimi nimeufanya moyo wake mzito, nipate kuzionesha ishara zangu hizi kati yao; 2 Kum 4:9;Zab 44:1;71:18;Yoe 1:3nawe upate kusema masikioni mwa mwanao, na masikioni mwa mjukuu wako, ni mambo gani niliyotenda juu ya Misri, na ishara zangu nilizozifanya kati yao; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA.