Maji toka mwambani
1 Hes 20:2-13;Kut 16:1;19:2;Hes 33:12,14 Mkutano wote wa wana wa Israeli ukasafiri, kutoka bara ya Sini kwa safari zao, kama BWANA alivyowaagiza, wakatua Refidimu; napo hapakuwa na maji, watu wanywe. 2 Hes 20:3;Kum 6:16;Zab 78:41;Isa 7:12;Mt 4:7;1 Kor 10:9 Kwa hiyo hao watu wakamgombeza Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwa nini mnanigombeza? Mbona mnamjaribu BWANA? 3 Kut 16:2 Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung’unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu? 4 1 Sam 30:6;Yn 8:59;10:31 Musa akamlilia BWANA, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe. 5 Eze 2:6;Hes 20:8 BWANA akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, ukawachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe; na ile fimbo yako ambayo uliupiga mto kwayo, uitwae mkononi mwako, ukaende. 6 Zab 105:41;114:8;1 Kor 10:4 Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli. 7 Zab 95:8;Ebr 3:8 Akapaita mahali pale jina lake Masa,17:7 Katika Kiebrania ni ‘jaribu’. na Meriba17:7 Katika Kiebrania ni ‘kunung’unika’. kwa sababu ya ugomvi wa wana wa Israeli, na kwa sababu walimjaribu BWANA, wakisema, Je! BWANA yu kati yetu au sivyo?
Waamaleki Washindwa na Waisraeli
8 Mwa 36:12;Hes 24:20;Kum 25:17;1 Sam 15:2 Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu. 9 Mdo 7:45;Ebr 4:8 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, uende ukapigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. 10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. 11 Yak 5:16 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda. 12 Lakini mikono ya Musa ililegea; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitengemaza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. 13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga. 14 Kum 25:17-19;1 Sam 15:2-9;Kut 34:27;1 Sam 30:1;2 Sam 8:12;Ezr 9:14 BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu. 15 Amu 6:24 Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi;17:15 Maana yake ni Bwana wangu au Mungu wangu ni Bendera yangu.16 akasema, BWANA ameapa;17:16 Maana katika Kiebrania si dhahiri. BWANA atakuwa na vita na Amaleki kizazi baada ya kizazi.