Publicidade

Êxodo 24

Damu ya Agano

1 Kut 28:1;Law 10:1,2;Hes 11:16 Kisha BWANA akamwambia Musa, Kweeni wewe, na Haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini wa wazee wa Israeli, mkamfikie BWANA; mkasujudie kwa mbali; 2 na Musa peke yake ndiye atakayekaribia karibu na BWANA; lakini hao hawatakaribia karibu; wala hao watu hawatakwea pamoja naye. 3 Musa akaenda akawaambia watu maneno yote ya BWANA, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena BWANA tutayatenda. 4 Kum 31:9;Mwa 28:18;31:45 Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya makabila kumi na mawili ya Israeli, 5 akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia BWANA sadaka za amani za ng’ombe. 6 Ebr 9:18 Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu. 7 Kisha akakitwaa Kitabu cha Agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda, nasi tutatii. 8 Mt 26:28;Mk 14:24;Lk 22:20;1 Kor 11:25;1 Pet 1:2;Ebr 9:19-20;10:29 Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya BWANA pamoja nanyi katika maneno haya yote.

Juu ya mlima: Utukufu wa Mungu waonekana

9 Ndipo akakwea juu, Musa, na Haruni, na Nadabu, na Abihu, na watu sabini miongoni mwa wazee wa Israeli; 10 Mwa 32:30;Kut 3:6;33:20,23;Isa 6:1,5;Yn 1:18;1 Tim 6:16;1 Yoh 4:12;Eze 1:26;10:1;Ufu 4:3;Mt 17:2 wakamwona Mungu wa Israeli; chini ya miguu yake palikuwa na kama sakafu iliyofanyizwa kwa yakuti samawi, kama zile mbingu zenyewe kwa usafi wake. 11 Kut 19:21;Mwa 16:13;Kum 4:33;Mwa 31:54;Kut 18:12 Naye hakuweka mkono wake juu ya hao wakuu wa wana wa Israeli; nao wakamwona Mungu, wakala na kunywa.

12 Kut 32:15;Kum 5:22 BWANA akamwambia Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku; nami nitakupa vibao vya mawe na ile sheria na hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe. 13 Kut 33:11 Musa akaondoka na Yoshua, mtumishi wake, Musa akapanda mlimani kwa Mungu. 14 Akawaambia hao wazee, Tungojeeni hapa, mpaka tutakaporudi kwenu; na tazameni, Haruni na Huri wapo pamoja nanyi; kila mtu aliye na jambo na awaendee. 15 Kut 19:9;Mt 17:5 Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima. 16 Kut 16:10;Hes 14:10 Na huo utukufu wa BWANA ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu. 17 Ebr 12:18 Na kuonekana kwake ule utukufu wa BWANA kulikuwa kama moto uteketezao, juu ya mlima machoni pa wana wa Israeli. 18 Kum 9:9 Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arubaini, mchana na usiku.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-04_23-13-58-