Mungu afunua jina lake takatifu
13 Kut 6:2-3;Mwa 32:29Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake ni nani? Niwaambie nini? 14 Ufu 1:4,8;Kut 6:3;Yn 8:58;Ebr 13:8Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;3:14 Au, Nitakuwa kama Nitakavyokuwa; au, Ndimi Ndiye. akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO3:14 Au, Nitakuwa; au, Ndimi. amenituma kwenu.