Publicidade

Ezequiel 2

Maono ya gombo

1 Dan 10:11 Akaniambia, Mwanadamu, simama kwa miguu yako, nami nitasema nawe. 2 Hes 11:25;Amu 13:25;Neh 9:30;Eze 3:24;Yoe 2:28,29 Naye aliposema nami, roho ikaniingia, ikanisimamisha; nikamsikia yeye aliyesema nami. 3 Yer 3:25 Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wameasi juu yangu, naam, hata hivi leo. 4 Eze 3:7 Na wana hao wana nyuso zisizo na haya, na mioyo yao ni migumu. Mimi nakutuma kwa hao; nawe utawaambia, Bwana MUNGU asema hivi. 5 Eze 3:11;33:33 Nao, iwe watasikia au hawataki kusikia, (maana ndio nyumba ya kuasi hao), hata hivyo watajua ya kuwa nabii amekuwako miongoni mwao. 6 Mt 10:28;Ebr 11:27;1 Pet 3:14;Eze 3:26,27 Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma inakuzunguka, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi. 7 Yer 1:7,17;Mt 28:20 Nawe utawaambia maneno yangu, iwe watasikia au hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana. 8 Ufu 10:9 Bali wewe, mwanadamu, sikia neno hili ninalokuambia; usiwe wewe mwenye kuasi kama nyumba ile yenye kuasi; funua kinywa chako, ule nikupacho. 9 Yer 1:9;Eze 3:1;Ufu 5:1 Nami nilipotazama, mkono ulinyoshwa kunielekea; na tazama, gombo la kitabu lilikuwa ndani yake. 10 Isa 3:11 Akalikunjua mbele yangu; nalo lilikuwa limeandikwa ndani na nje; ndani yake yalikuwa yameandikwa maombolezo, na vilio, na ole!

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-