30 Ufu 21:12-13Na matokeo ya mji ndiyo haya; upande wa kaskazini, mianzi elfu nne na mia tano, kwa kipimo; 31 Isa 60:18;Ufu 21:12na malango ya mji yatatajwa kwa majina ya makabila ya Israeli, malango matatu upande wa kaskazini; lango la Reubeni, moja; lango la Yuda, moja; na lango la Lawi, moja. 32 Na upande wa mashariki, mianzi elfu nne na mia tano, kwa kipimo; na malango matatu; lango la Yusufu, lango la Benyamini; lango la Dani. 33 Na upande wa kusini, mianzi elfu nne na mia tano kwa kupima; na malango matatu; lango la Simeoni; lango la Isakari, lango la Zabuloni. 34 Na upande wa magharibi, mianzi elfu nne na mia tano; pamoja na malango yake matatu; lango la Gadi, lango la Asheri; na lango la Naftali.
Ezekieli 48:30-34
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
30 "Haya yatakuwa ndiyo malango ya mji ya kutokea:
"Kuanzia upande wa kaskazini, ambayo urefu wake ni dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu, 31 malango hayo ya mji yatapewa majina ya makabila ya Israeli. Malango hayo matatu ya upande wa kaskazini moja litakuwa lango la Reubeni, lango la Yuda na lango la Lawi.
32 Upande wa mashariki, wenye urefu wa dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu: lango la Yusufu, lango la Benyamini na lango la Dani.
33 Upande wa kusini, wenye urefu wa dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu: lango la Simeoni, lango la Isakari na lango la Zabuloni.
34 Upande wa magharibi, wenye urefu wa dhiraa elfu nne na mia tano, utakuwa na malango matatu: lango la Gadi, lango la Asheri na lango la Naftali.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
30 "Haya yatakuwa ndiyo malango ya mji ya kutokea: Kuanzia upande wa kaskazini, ambayo urefu wake ni dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu, 31 malango hayo ya mji yatapewa majina ya makabila ya Israeli. Malango hayo matatu ya upande wa kaskazini moja litakuwa lango la Reubeni, lango la Yuda na lango la Lawi.
32 "Upande wa mashariki, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Yosefu, lango la Benyamini na lango la Dani.
33 "Upande wa kusini, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Simeoni, lango la Isakari na lango la Zabuloni.
34 "Upande wa magharibi, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Gadi, lango la Asheri na lango la Naftali.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.