Yuda ajinyonga
3 Mdo 1:18-19;Mt 26:15Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nilikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia. 4 Wakasema, Basi, haya yatuhusu nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.