1 Ikawa katika mwaka wa nne wa mfalme Dario, neno la BWANA lilimjia Zekaria, siku ya nne ya mwezi wa tisa, yaani, Kislevu. 2 Basi watu wa Betheli walikuwa wamewatuma Shareza na Regem-meleki, na watu wao, ili kuomba fadhili za BWANA, 3 Kum 17:9;Mal 2:7 na kusema na makuhani wa nyumba ya BWANA wa majeshi, na hao manabii, ya kwamba, Je! Yanipasa kulia katika mwezi wa tano, na kufunga, kama nilivyofanya miaka hii mingi iliyopita? 4 Ndipo neno la BWANA wa majeshi likanijia, kusema, 5 Zek 1:12;2 Fal 25:25;Isa 58:4;Mt 6:16;Rum 14:6 Waambie watu wote wa nchi, na hao makuhani, ukisema, Hapo mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano7:5 mfungo wa mwezi wa tano ulikuwa wa kukumbuka kushindwa kwa Yerusalemu katika mwaka wa 487 K.K. na mwezi wa saba,7:5 mfungo wa mwezi wa saba ulikuwa wa kukumbuka kuuawa kwa Jedalia, mtawala. katika miaka hiyo sabini, je, Mlifunga kwa ajili yangu? 6 Na wakati mnapokula chakula na kunywa, je, Hamli kwa ajili ya nafsi zenu, na kunywa kwa ajili ya nafsi zenu? 7 Yer 17:26 Je, Hayo siyo maneno aliyoyasema BWANA kwa vinywa vya manabii wa zamani, wakati Yerusalemu ulipokaliwa na watu na kufanikiwa, na miji yake iliyokuwa ikiuzunguka; na wakati ule ambao nchi ya Negebu na Shefela ilipokuwa ikikaliwa na watu?
8 Kisha neno la BWANA likamjia Zekaria, kusema, 9 BWANA wa majeshi amesema hivi, ya kwamba, Fanyeni hukumu za kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma; 10 tena msimdhulumu mjane, wala yatima, wala mgeni, wala maskini; wala mtu awaye yote miongoni mwenu asiwaze mabaya juu ya ndugu yake moyoni mwake. 11 Lakini hao walikataa kusikiliza, wakageuza bega lao, wakaziba masikio yao ili wasisikie. 12 Naam, walifanya mioyo yao kuwa kama jiwe gumu, wasije wakaisikia sheria na maneno ya BWANA wa majeshi, aliyoyatuma kwa roho yake, kwa mkono wa manabii wa kwanza; kwa sababu hiyo ghadhabu kuu ikatoka kwa BWANA wa majeshi. 13 Ikawa kama wakati nilipowaita, wasitake kunisikiliza; basi, nao wataniita, wala sitasikiliza, asema BWANA wa majeshi. 14 Lakini nitawatawanya kwa kimbunga kikali katikati ya mataifa yote wasiyoyajua. Basi nchi walioacha ikawa ya ukiwa, hata hapakuwa na mtu aliyeipitia akienda wala akirudi; maana waliifanya nchi iliyopendeza kuwa ukiwa.