Publicidade

Gravidez e maternidade

Por Bíblia Online

Gravidez e maternidade são bênçãos celebradas na Bíblia. Deus forma cada criança no ventre, cuida da mãe e da família, e abençoa a geração dos justos.

Filhos são herança do Senhor

Deus abençoa a fertilidade e o crescimento das famílias. Cada criança é obra de suas mãos, conhecida e amada antes mesmo de nascer.

Utabarikiwa kuliko mataifa yote; hakutakuwa na mwanamume wala mwanamke aliye tasa kati yenu; wala kati ya wanyama wenu wa kufugwa.

Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.

Wazawa wake watakuwa hodari duniani;

Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.

Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,

Uliniunga tumboni mwa mama yangu.

Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa

Kwa njia ya ajabu ya kutisha.

Matendo yako ni ya ajabu,

Na nafsi yangu yajua sana,

Mifupa yangu haikusitirika kwako,

Nilipoumbwa kwa siri,

Nilipoungwa kwa ustadi katika pande za chini za nchi;

Macho yako yaliniona kabla sijakamilika;

Kitabuni mwako ziliandikwa zote pia,

Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.

Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA,

Uzao wa tumbo ni thawabu.

Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako.

Força e cuidado na gravidez

Deus dá forças à mulher grávida e a sustenta em cada etapa. Sua graça é suficiente e seu poder se aperfeiçoa na fraqueza.

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

Unitegee sikio lako, uniokoe hima.

Uwe kwangu mwamba wa nguvu,

Ngome thabiti ya kuniokoa.

Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo,

Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.

Atalilisha kundi lake kama mchungaji,

Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake;

Na kuwachukua kifuani mwake,

Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Nisikilizeni, enyi wa nyumba ya Yakobo, ninyi mlio mabaki ya nyumba ya Israeli, mliochukuliwa nami tangu tumboni, mlioinuliwa tangu mimbani; na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.

A bênção da maternidade

A Bíblia honra a maternidade como ministério sagrado. As mães são instrumentos de Deus para formar vidas e transmitir a fé.

Lakini ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.

Wanawe huondoka na kumwita heri;

Mumewe naye humsifu, na kusema,

Kaini amwua Habili

Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto wa kiume kwa msaada wa BWANA.

Kuzaliwa kwa Isaka

BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema. Sara akapata mimba akamzalia Abrahamu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.

Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.

Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume; akamwita Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA.

Proteção divina

Deus protege a mãe e o bebê, guardando-os de todo mal. Ele acompanha cada momento com ternura e fidelidade.

Hakikisho la ulinzi wa Mungu

Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu

Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu nitakayemtumaini.

BWANA atakulinda na mabaya yote,

Atakulinda nafsi yako.

BWANA atakulinda utokapo na uingiapo,

Tangu sasa na hata milele.

Kabla sijakuumba katika tumbo nilikujua, na kabla hujatoka tumboni, nilikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Watu wanaume wakipigana, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema. Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai,

Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe.

Esperança e promessa

A maternidade é caminho de esperança. Como Sara, Ana e Isabel, as mães encontram na fé a força para aguardar as promessas de Deus.

Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.

Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.

Wimbo wa Sifa wa Mariamu

Mariamu akasema,

Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;

Kwa kuwa ameutazama

Unyonge wa mjakazi wake.

Kwa maana, tazama, tokea sasa

Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;

Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,

Na jina lake ni takatifu.

Humweka nyumbani mwanamke aliye tasa,

Awe mama ya watoto mwenye furaha.

Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa makabila ya watu watatoka kwake.

Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,

Katika nyumba yako.

Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni

Wakiizunguka meza yako.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-