Publicidade

Salmos 61

Hakikisho la ulinzi wa Mungu

Kwa mwimbishaji: kwa ala za nyuzi za muziki. Ya Daudi.

1 Ee Mungu, ukisikie kilio changu,

Uyasikilize maombi yangu.

2 1 Tim 2:8 Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo,

Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.

3 Mit 18:10 Kwa maana ulikuwa kimbilio langu,

Ngome yenye nguvu adui asinipate.

4 Zab 15:1;23:6;Ufu 3:12 Nitakaa katika hema yako milele,

Na kupata kimbilio chini ya mbawa zako.

5 1 Kor 3:21-23 Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu.

Umewapa urithi wao waliogopao jina lako.

6 Utaziongeza siku za mfalme,

Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.

7 Zab 41:12;Lk 1:32 Atakaa mbele za Mungu milele,

Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.

8 Zab 56:12 Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima,

Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-