1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
3 Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji,
Na katika maradhi mabaya.
4 Zab 61:4 Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Ayu 5:19;Mit 3:23;Isa 43:2 Hutaogopa hatari za usiku,
Wala mshale urukao mchana,
6 Wala mapigo yajayo usiku,
Wala maafa yatokeayo adhuhuri,
7 Hata watu elfu wakianguka ubavuni pako.
Naam, watu elfu kumi katika mkono wako wa kulia!
Wewe hutakaribiwa na maafa.
8 Mal 1:5 Ila kwa macho yako utatazama,
Na kuyaona malipo ya wasio haki.
9 Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;
Umemfanya Aliye Juu kuwa makao yako.
10 Mit 1:33;2 The 3:3;2 Pet 2:9 Mabaya hayatakupata wewe,
Wala tauni haitaikaribia hema yako.
11 Mt 4:6;Lk 4:10 Kwa kuwa atakuagizia malaika wake
Wakulinde katika njia zako zote.Zab 34:7;Mt 4:6;Lk 4:10;Ebr 1:14
12 Ayu 5:23;Zab 37:24;Mt 4:6;Lk 4:11 Mikononi mwao watakuchukua,
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
13 Lk 10:19 Utawakanyaga simba na nyoka,
Mwanasimba na joka utawakanyaga kwa miguu.
14 Kwa kuwa amekaza kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,
Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ayu 22:27;Zab 18:3;Yer 33:3;Zek 13:9;Ebr 5:7;Zab 43:2;1 Sam 2:30 Ataniita nami nitamwitikia;
Nitakuwa pamoja naye taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza;
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha,
Nami nitamwonesha wokovu wangu.