Pular para o conteúdo
Publicidade

Protecção e segurança

Por Bíblia Online

Deus é nosso protetor e refúgio seguro. Em todas as circunstâncias, a Bíblia nos assegura que o Senhor guarda, sustenta e protege aqueles que nele confiam.

Deus, a nossa fortaleza

O Senhor é refúgio e fortaleza, socorro bem presente na angústia. Quem habita no esconderijo do Altíssimo descansa à sombra do Todo-Poderoso.

Ulinzi wa Mungu kwa mji na watu wake

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Ulinzi wa Mungu kwa mji na watu wake

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Hakikisho la ulinzi wa Mungu

Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu

Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu nitakayemtumaini.

Kwa manyoya yake atakufunika,

Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;

Uaminifu wake ni ngao na kigao.

Hata watu elfu wakianguka ubavuni pako.

Naam, watu elfu kumi katika mkono wako wa kulia!

Wewe hutakaribiwa na maafa.

Kwa kuwa Wewe BWANA ndiwe kimbilio langu;

Umemfanya Aliye Juu kuwa makao yako.

Mabaya hayatakupata wewe,

Wala tauni haitaikaribia hema yako.

Wimbo wa ushindi katika Bwana wa Daudi

BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu,

Nimwogope nani?

BWANA ni ngome ya uzima wangu,

Nimhofu nani?

Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,

Ngome yangu, sitatikisika.

BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa,

Naam, ngome kwa nyakati za shida.

O escudo do Senhor

Deus nos rodeia com sua proteção como um escudo. Ele é rocha, baluarte e libertador. Sua fidelidade nos cobre e nos guarda.

Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,

Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.

Mwamini Mungu katika dhiki

BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,

Ni wengi wanaonishambulia,

Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,

Hana wokovu huyu kwa Mungu.

Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,

Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.

Kwa sauti yangu namwita BWANA

Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.

Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena,

Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.

Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu,

Waliojipanga Juu yangu pande zote.

Mungu, njia yake ni kamilifu,

Ahadi ya BWANA imehakikishwa,

Yeye ndiye ngao yao.

Wote wanaomkimbilia.

Nawe umenipa ngao ya wokovu wako,

Mkono wako wa kulia umenitegemeza,

Na unyenyekevu wako umenikuza.

Umezipanulia nafasi hatua zangu,

Na miguu yangu haikuteleza.

Sala kwa ukombozi wa kitaifa na usalama

Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu,

Aifundishaye mikono yangu vita,

Na vidole vyangu kupigana.

Mwamba wangu na ngome yangu,

Nguzo yangu na mwokozi wangu

Ngao yangu ninayemkimbilia,

Huwatiisha watu wangu chini yangu.

Awapaye wafalme wokovu,

Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.

Nao wote wanaokukimbilia watafurahi;

Watapiga kelele za furaha daima.

Kwa kuwa Wewe unawahifadhi,

Walipendao jina lako watakufurahia.

Kwa maana Wewe utambariki mwenye haki;

BWANA, utamzungushia radhi kama ngao.

Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,

Utege sikio lako ulisikie neno langu.

Dhihirisha fadhili zako za ajabu

Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia;

Kwa mkono wako wa kulia

Uwaokoe kutoka kwa adui zao.

Unilinde kama mboni ya jicho,

Unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako;

Wasinione wasio haki wanaonionea,

Adui za roho yangu wanaonizunguka.

Kwa kuwa mfalme humtumainia BWANA,

Na kwa fadhili zake Aliye Juu hatatikisika.

Mkono wako utawapata adui zako wote,

Mkono wako wa kulia utawapata wanaokuchukia.

Utawafanya kuwa kama tanuri ya moto,

Wakati wa ghadhabu yako.

BWANA atawameza kwa ghadhabu yake,

Na moto utawateketeza.

Kimbilio langu utanilinda nisipate mateso,

Utanizungusha nyimbo za kufurahia wokovu wangu.

Segurança e provisão

O Senhor supre todas as necessidades dos seus filhos. Quem busca o Reino primeiro não precisa temer — nada faltará aos que temem ao Senhor.

Mchungaji mwema

BWANA ndiye mchungaji wangu,

Sitapungukiwa na kitu.

Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa;

Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.

Umtumaini BWANA ukatende mema,

Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.

Nilikuwa kijana na sasa ni mzee,

Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa

Wala mzawa wake akiomba chakula.

Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.

Omba, tafuta, bisha

Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.

Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?

Guarda e livramento

O anjo do Senhor acampa ao redor dos que o temem e os livra. Deus promete guardar todas as nossas saídas e entradas para sempre.

Malaika wa BWANA huwazungukia,

Wamchao na kuwaokoa.

BWANA huzikomboa nafsi za watumishi wake,

Wote wamkimbiliao hawatahukumiwa.

Hakikisho la ulinzi wa Mungu

Nayainua macho yangu niitazame milima,

Msaada wangu utatoka wapi?

Msaada wangu hutoka kwa BWANA,

Aliyezifanya mbingu na nchi.

Hatauacha mguu wako usogezwe;

Akulindaye hatasinzia;

Naam, hatasinzia wala hatalala,

Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

BWANA ndiye mlinzi wako;

BWANA ni uvuli katika mkono wako wa kulia.

Jua halitakupiga mchana,

Wala mwezi wakati wa usiku.

BWANA atakulinda na mabaya yote,

Atakulinda nafsi yako.

BWANA atakulinda utokapo na uingiapo,

Tangu sasa na hata milele.

Wimbo wa imani na usalama kwa Mungu

Mungu, unihifadhi mimi,

Kwa maana nakukimbilia Wewe.

Wimbo wa imani na usalama kwa Mungu

Mungu, unihifadhi mimi,

Kwa maana nakukimbilia Wewe.

Nimemweka BWANA mbele yangu daima,

Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa.

Nimemweka BWANA mbele yangu daima,

Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa.

Sala ya ushindi

BWANA akujibu siku ya dhiki,

Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.

Akutumie msaada toka patakatifu pake,

Na kukutegemeza toka Sayuni.

Unilinde nafsi yangu na kuniokoa,

Usiniache niaibike, maana nakukimbilia Wewe.

Ukamilifu na unyofu zinihifadhi,

Maana nakungoja Wewe.

Farasi hafai kitu kwa wokovu,

Wala hamponyi mtu kwa wingi wa nguvu zake.

Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao,

Wazingojeao fadhili zake.

Ili kuwaponya nafsi zao kutoka kwa mauti,

Na kuwahuisha wakati wa njaa.

Nafsi zetu zinamngoja BWANA;

Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.

Confiança inabalável

Melhor é confiar no Senhor do que confiar no homem. Quem anda em integridade anda seguro, e a torre forte do nome do Senhor protege o justo.

BWANA yuko upande wangu, sitaogopa;

Mwanadamu atanitenda nini?

Ni heri kumkimbilia BWANA

Kuliko kuwatumainia wanadamu.

Jina la BWANA ni ngome imara;

Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.

Jina la BWANA ni ngome imara;

Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.

Kumcha BWANA ni tumaini imara;

Watoto wake watakuwa na kimbilio.

Kwa kuwa BWANA atakuwa tumaini lako,

Naye atakulinda mguu wako usinaswe.

Aendaye kwa unyofu huenda salama;

Bali apotoshaye njia zake atajulikana.

Kila neno la Mungu limehakikishwa;

Yeye ni ngao yao wamwaminio.

Kila neno la Mungu limehakikishwa;

Yeye ni ngao yao wamwaminio.

Haki humlinda yeye aliye mnyofu katika njia yake;

Bali ubaya humwangusha mwenye dhambi.

Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake;

Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa.

Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima;

Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;

Huwawekea wanyofu akiba ya hekima kamili;

Yeye ni ngao kwao waendao kwa ukamilifu;

Apate kuyalinda mapito ya hukumu,

Na kuhifadhi njia ya watakatifu wake.

Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha;

Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.

Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita;

Lakini BWANA ndiye aletaye wokovu.

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;

Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

A presença protetora

O Senhor prometeu estar conosco e nunca nos desampara. Ele é como sombra à nossa direita e fortaleza em todo o tempo.

Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia wala kukuacha.

Mungu wa milele ndiye makazi yako,

Na mikono ya milele i chini yako.

Na mbele yako amemsukumia mbali adui;

Akasema, Angamiza.

Akamnena Benyamini,

Mpenzi wa BWANA atakaa salama kwake;

Yuamfunika mchana kutwa,

Naye hukaa kati ya mabega yake.

Kila silaha itengenezwayo juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.

Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea

Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.

Kama ndege warukao, BWANA wa majeshi ataulinda Yerusalemu; ataulinda na kuuokoa, atapita juu yake na kuuhifadhi.

jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.

Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.

BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.

BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.

Promessas de cuidado

Deus garante que nem um fio de cabelo cairá sem sua permissão. Ele deseja que vivamos em paz, confiança e segurança total nele.

Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu; lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi.

Na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.

Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. Lakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu. Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.

Mfuko, mkoba, na upanga

Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!

Upendo wa Mungu katika Kristo Yesu

Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?

Hata tunathubutu kusema,

Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa;

Mwanadamu atanitenda nini?

Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.

Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.

Fidelidade e aliança

Deus é fiel à sua aliança. Ele protege cada promessa que faz e guarda os seus como a menina dos seus olhos.

Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu.

na lolote tuombalo, tunalipokea kwake, kwa kuwa tunazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.

Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tunapoomba chochote, tunajua kwamba tumetimiziwa zile haja tulizomwomba.

Tunajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.

Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. Nilipokuwapo pamoja nao, mimi niliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.

Maana ni nani aliye Mungu, ila BWANA?

Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu?

basi, sasa, uwe radhi, ukaibariki nyumba ya mtumishi wako, ipate kudumu milele mbele zako; kwa maana wewe, Ee Bwana MUNGU, umelinena na kwa baraka yako nyumba ya mtumishi wako na ibarikiwe milele.

Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.

nami nimekuwa pamoja nawe kila ulikokwenda, na kuwakatilia mbali adui zako wote mbele yako; nami nitakufanyia jina, kama jina la hao wakuu walioko duniani.

Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama.

Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.

Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

Provisão diária

Deus satisfaz os desejos do coração dos seus filhos. Ele abençoa, renova as forças e sustenta dia após dia quem nele confia.

Nawe, BWANA, usinizuilie rehema zako,

Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.

Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza,

Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.

Nami nitaimba juu ya nguvu zako,

Nitaimba kwa furaha juu ya fadhili zako asubuhi.

Maana umekuwa ngome yangu,

na kimbilio wakati wa mateso yangu.

Bali mfalme atamfurahia Mungu,

Kila aapaye kwa Yeye atashangilia,

Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.

Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,

Mwimbieni wimbo yeye apitaye katika mawingu,

Jina lake ni YAHU;

Shangilieni mbele zake.

Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,

Ni Mungu aliye katika kao lake takatifu.

Na ahimidiwe Bwana,

Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu;

Mungu ndiye wokovu wetu.

Mimi ndimi BWANA, Mungu wako,

Niliyekupandisha toka nchi ya Misri;

Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.

Kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao,

BWANA atatoa neema na utukufu.

Hatawanyima kitu chema

Hao waendao kwa ukamilifu.

Enyi mmpendao BWANA, uchukieni uovu;

Huwalinda nafsi zao watauwa wake,

Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki.

BWANA huwalinda wasio na hila;

Nilidhilika, akaniokoa.

Ee nafsi yangu, urudi pumzikoni mwako,

Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.

Maana umeniponya nafsi yangu na mauti,

Macho yangu na machozi,

Na miguu yangu na kuanguka.

Nitaenenda mbele za BWANA

Katika nchi za walio hai.

Ndiwe sitara yangu na ngao yangu,

Neno lako nimelingojea.

Baraka za Mungu nyumbani

BWANA asipoijenga nyumba

Waijengao wanafanya kazi bure.

BWANA asipoulinda mji

Yeye aulindaye anakesha bure.

Hapo nitamchipushia Daudi pembe,

Na taa nimemtengenezea masihi wangu.

Adui zake nitawavika aibu,

Bali juu yake taji lake litasitawi.

BWANA atanitimizia malengo yake kwangu;

Ee BWANA, fadhili zako ni za milele;

Usiiache kazi ya mikono yako.

Waufumbua mkono wako,

Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.

Huwafanyia hukumu walioonewa,

Huwapa wenye njaa chakula;

BWANA hufungua waliofungwa;

BWANA huwafumbua macho waliopofuka;

BWANA huwainua walioinama;

BWANA huwapenda wenye haki;

BWANA huwahifadhi wageni;

Huwategemeza yatima na mjane;

Bali njia ya wasio haki huiharibu.

Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara,

Maana Wewe, BWANA, peke yako,

Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.

Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Msimwibie Mungu

Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka.

Kwa maana ulinzi wa hekima ni kama ulinzi wa fedha na ubora wa maarifa ni kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.

Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.

Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.

Kwa maana nimeishibisha roho yenye uchovu, nami nimeiridhisha kila roho yenye huzuni.

Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, lakini sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.

Seja o primeiro