Publicidade

Salmos 138

Shukrani na sifa ya Daudi

1 Zab 119:46 Nitakushukuru kwa moyo wangu wote,

Mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.

2 1 Fal 8:29;Zab 5:7;Dan 6:10;Yon 2:7;Isa 42:21 Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu,

Nitalishukuru jina lako,

Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako,

Kwa maana umeikuza ahadi yako,

na jina lako juu ya vyote.

3 2 Kor 12:9;Zek 10:12 Siku ile niliyokuita uliniitikia,

Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.

4 Ee BWANA, wafalme wote wa dunia watakushukuru,

Watakapoyasikia maneno ya kinywa chako.

5 Naam, wataziimba njia za BWANA,

Kwa maana utukufu wa BWANA ni mkuu.

6 Mit 3:34;Yak 4:6 Ingawa BWANA yuko juu, anamjali mnyenyekevu,

Naye amjua mwenye kujivuna tokea mbali.

7 Zab 23:3 Nijapopitia katika shida,

Unanilinda juu ya hasira ya adui zangu,

Unaunyosha mkono wako,

Na mkono wako wa kulia unaniokoa.

8 Zab 57:2;Flp 1:6 BWANA atanitimizia malengo yake kwangu;

Ee BWANA, fadhili zako ni za milele;

Usiiache kazi ya mikono yako.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-