1 Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:
2 Kwa kupata hekima na nidhamu;
kwa kufahamu maneno ya busara;
3 kwa kujipatia nidhamu na busara,
kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;
4 huwapa busara wajinga1:4 Neno la Kiebrania lililotafsiriwa mjinga (wingi wajinga) linamaanisha mtu anayeamini chochote, asiye na maadili, na mwenye roho ya kutenda uovu.,
maarifa na akili kwa vijana;
5 wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,
wenye kupambanua na wapate mwongozo;
6 kwa kufahamu mithali na mifano,
misemo na vitendawili vya wenye hekima.
7 Kumcha Mwenyezi Mungu ni chanzo cha maarifa,
lakini wapumbavu1:7 Neno la Kiebrania lililotafsiriwa mpumbavu (wingi wapumbavu) linamaanisha mtu asiye na maadili. hudharau hekima na adabu.