25 Amevikwa nguvu na heshima,
anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo.
26 Huzungumza kwa hekima,
na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.
27 Huangalia mambo ya nyumbani mwake
wala hali chakula cha uvivu.
28 Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa,
mumewe pia humsifu, akisema:
29 "Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri,
lakini wewe umewapita wote."
30 Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu,
na uzuri unapita upesi;
bali mwanamke anayemcha Mwenyezi Mungu atasifiwa.