Maonyo dhidi ya upumbavu
1 Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako,
ikiwa umeshikana mikono kwa kuweka ahadi
kwa ajili ya mwingine,
2 kama umetegwa na ulichosema,
umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,
3 basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru,
kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako:
Nenda ukajinyenyekeshe kwake;
msihi jirani yako!
4 Usiruhusu usingizi machoni pako,
usiruhusu kope zako zisinzie.
5 Jiweke huru, kama paa kutoka mkononi mwa mwindaji,
kama ndege kutoka mtego wa mwindaji.