Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Mambo ya Nyakati 20

Kuzingirwa na kutekwa kwa Raba

1 2 Sam 11:1;1 Fal 20:22;2 Nya 36:10;Mhu 3:8;2 Sam 12:26;Yer 49:2;Eze 21:20 Hata ikawa, mwanzo wa mwaka mpya, wakati watokapo wafalme kwenda vitani, Yoabu akawaongoza mashujaa wa jeshi, akaiteka nyara nchi ya wana wa Amoni, akaja akauzingira Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu. Naye Yoabu akaupiga Raba akauangamiza. 2 2 Sam 12:30,31 Kisha Daudi akatwaa taji la Milkomu20:2 Katika makala zingine ni mfalme wao. toka kichwani pake, akaona ya kwamba uzani wake ni talanta ya dhahabu, na kulikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani; akazitoa nyara za mji, nyingi sana. 3 Na hao watu waliokuwamo akawatoa, akawawafanyisha kazi kwa misumeno, na kwa sululu za chuma, na kwa mashoka. Ndivyo alivyofanya Daudi kwa miji yote ya wana wa Amoni. Nao wakarudi Yerusalemu Daudi na watu wote.

Kushindwa kwa Wafilisti

4 Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gezeri; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai;20:4 Au, wana wa jitu. nao Wafilisti20:4 Katika Kiebrania hakuna Wafilisti. wakashindwa. 5 Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi,20:5 Au, Mbethlehemi akamwua nduguye Goliathi. Mgiti, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji. 6 Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai.20:6,8 Au, huyu jitu.7 Naye huyo alipowatukana Israeli, Yonathani, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua. 8 Hao walizaliwa kwake huyo Mrefai20:6,8 Au, huyu jitu. wa Gathi, nao wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mkono wa watumishi wake.

Veja também