10 Kut 37:1;Kum 10:3;Ebr 9:4Nao na wafanye sanduku la mti wa mjohoro; urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa25:10 Ni urefu wa kutoka kiwiko cha mkono hadi ncha ya kidole kirefu. moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu. 11 Nawe ulifunike kwa dhahabu safi, ulifunike ndani na nje, nawe tia na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote. 12 Nawe subu vikuku vinne vya dhahabu kwa ajili yake, na kuvitia katika miguu yake minne; vikuku viwili upande mmoja, na vikuku viwili upande wake wa pili. 13 Nawe fanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu. 14 Nawe tia hiyo miti katika vile vikuku vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku. 15 1 Fal 8:8Hiyo miti itakaa katika vile vikuku vya sanduku; haitaondolewa. 16 Kut 16:34;31:18;40:20;Kum 10:2;31:26;1 Fal 8:9;2 Fal 11:12Kisha tia ndani ya sanduku huo ushuhuda nitakaokupa. 17 Ebr 9:5;Kut 37:6;Rum 3:25Nawe fanya kiti cha rehema25:17 Agano au ‘kifuniko’. cha dhahabu safi; urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. 18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi yawe kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku. 20 1 Fal 8:7;1 Nya 28:18Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Kut 26:34;40:20Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku.
Publicidade