Adoração
A adoração é a resposta do coração humano à majestade de Deus. Deus é Espírito e importa que os que o adoram o adorem em espírito e em verdade — com todo o ser.
Adorar em espírito
Deus é Espírito e importa que os adoradores o adorem em espírito e em verdade. A adoração verdadeira brota do coração.
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.
Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.
Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Maisha mapya katika Kristo
Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
Maisha mapya katika Kristo
Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.
Kwa kuwa imeandikwa,
Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu;
Na kila ulimi utamkiri Mungu.
Louvor e reverência
Vinde, adoremos e prostremo-nos. Louvai ao Senhor! Todo ser que respira louve o nome glorioso do Senhor.
Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.
Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.
Sifa kwa ukuu Mwingi wa Mungu
Haleluya.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake;
Msifuni katika anga la uweza wake.
Msifuni kwa matendo yake makuu;
Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
Msifuni kwa mvumo wa baragumu;
Msifuni kwa kinanda na kinubi;
Msifuni kwa matari na kucheza;
Msifuni kwa zeze na filimbi;
Msifuni kwa matoazi yaliayo;
Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.
Haleluya.
Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.
Haleluya.
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.
Sifa kwa ajili ya wema wa Mungu kwa Israeli
Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
Imbeni utukufu wa jina lake,
Tukuzeni sifa zake.
Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini!
Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako,
Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
Nchi yote itakusujudia na kukuimbia,
Naam, italiimbia jina lako.
Nilimwita kwa kinywa changu,
Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu.
Mataifa yote uliyoyaumba watakuja;
Watakusujudia Wewe, Bwana,
Watalitukuza jina lako;
Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu,
Wewe ndiwe mfanya miujiza,
Ndiwe Mungu peke yako.
Shukrani kwa wema wa Mungu
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
Uaminifu wa Mungu kwa Israeli
Haleluya.
Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake,
Wajulisheni watu matendo yake.
Faraja na uhakikisho katika Bwana
Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu,
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;
Midomo yangu itakusifu.
Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;
Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Declarações de adoração
Tu és digno, Senhor, de receber glória e honra! Ao Senhor pertence a grandeza, o poder, a glória e a majestade.
Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kuupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.
akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
Hitimisho na baraka
Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nilianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionesha hayo. Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.
Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Nanyi semeni,
Ee Mungu wa wokovu wetu, utuokoe,
Utukusanye kwa kututoa katika mataifa,
Tulishukuru jina lako takatifu,
Tuzifanyie shangwe sifa zako.
Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA.
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Mwimbieni, mwimbieni nyimbo za kumsifu;
Yatangazeni matendo yake yote ya ajabu.
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Sacrifício de louvor
Por meio de Jesus ofereçamos sempre sacrifício de louvor. Cantai ao Senhor, celebrai em salmos — enchei-vos do Espírito.
Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamalo jina lake.
Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na muwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho; maana Mungu wetu ni moto ulao.
mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Lakini ilipokuwa karibu usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
Shukrani za Paulo baada ya dhiki
Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.
hilo tuliloliona na kulisikia, tunawahubiria na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
Adoração como vida
Exaltai ao Senhor, prostrai-vos ante o escabelo dos seus pés. A adoração genuína transforma o adorador e agrada o Criador.
Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;
Sujuduni penye kiti cha miguu yake;
Ndiye mtakatifu.
Kinywa changu kitajazwa sifa zako,
Na heshima yako mchana kutwa.
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,
Mwimbieni wimbo yeye apitaye katika mawingu,
Jina lake ni YAHU;
Shangilieni mbele zake.
Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,
Ni Mungu aliye katika kao lake takatifu.
Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake;
Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu.
Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu,
Katikati ya kusanyiko nitakusifu.
Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni,
Enyi nyote mlio wazawa wa Yakobo, mtukuzeni,
Mcheni, enyi nyote mlio wazawa wa Israeli.
Nakunyoshea mikono yangu;
Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama,
Na kufadhaika ndani yangu?
Umtumaini Mungu;
Kwa maana nitakuja kumsifu,
Aliye afya ya uso wangu,
Na Mungu wangu.
Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu;
Sina wema ila utokao kwako.
Mtumikieni BWANA kwa kicho,
Shangilieni kwa kutetemeka.
Nitafurahi na kukushangilia;
Nitaliimbia sifa jina lako, Wewe Uliye juu.
Falsa adoração
Não terás outros deuses diante de mim. Não adorarás ídolos. A adoração exclusiva ao Senhor é mandamento inegociável.
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Maana hutamwabudu mungu mwingine, kwa kuwa BWANA, ambaye jina lake ni mwenye wivu, ni Mungu mwenye wivu.
Ikawa Musa alipoingia humo hemani, ile nguzo ya wingu ikashuka, ikasimama mlangoni pa ile hema; naye BWANA akasema na Musa. Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake.
BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu;
Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe?
Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu,
Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?
Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.
Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.
na huko mtakula mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi furahini katika yote mtakayotia mikono yenu, ninyi na wa nyumbani mwenu, aliyokubarikia BWANA, Mungu wako.
Wakamtia wivu kwa miungu migeni,
Wakamkasirisha kwa machukizo.
Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu,
Kwa miungu wasiyoijua,
Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu,
Ambayo baba zenu hawakuiogopa.
Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa,
Mungu aliyekuzaa umemsahau.
Jitunzeni nafsi zenu, mioyo yenu isije ikadanganywa, mkageuka na kutumikia miungu mingine na kuiabudu;
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;
Sifa kwa kukombolewa katika udhalimu
Ee BWANA, wewe u Mungu wangu;
Nitakutukuza na kulihimidi jina lako;
Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu,
Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.
Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii,
Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka
Miaka arubaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?
Nanyi mlichukua hema ya Moleki,
Na nyota za mungu wenu Refani,
Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu;
Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.
Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili; wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukineemeshwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kama atakavyo Mungu.
Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama cha kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
Exemplos de adoração
Jó adorou em meio ao sofrimento. Esdras adorou na restauração. Paulo e Silas adoraram na prisão — e Deus respondeu.
Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kusujudia; akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vile vile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
Wakaimbiana, wakimhimidi BWANA, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA umekwisha kuwekwa.
Basi mimi, Nebukadneza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili.
Kwa hiyo, wewe ndiwe mkuu, Ee BWANA Mungu, kwa maana hakuna kama wewe, wala hapana Mungu mwingine ila wewe, kwa kadiri tulivyosikia kwa masikio yetu.
Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA;
Kwa maana hakuna yeyote ila wewe,
Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
Ndipo Walawi, Yeshua na Kadmieli, na Bani, na Hashabneya, na Sherebia, na Hodia, na Shebania, na Pethahia, wakasema, Simameni, mkamhimidi BWANA, Mungu wenu, tangu milele na hata milele. Na lihimidiwe jina lako tukufu, lililotukuka kuliko baraka zote na sifa zote.
Imani na shangwe katika shida
Maana mtini hautachanua maua,
Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda;
Taabu ya mzeituni itakuwa bure,
Na mashamba hayatatoa chakula;
Zizini hamtakuwa na kundi,
Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng’ombe;
Walakini nitamfurahia BWANA
Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.
Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.