Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 29

Sauti ya Mungu katika dhoruba

Zaburi ya Daudi.

1 Zab 96:7-9;1 Nya 16:28,29 Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu,

Mpeni BWANA utukufu na nguvu;

2 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;

Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.

3 Sauti ya BWANA inasikika juu ya maji;

Mungu wa utukufu apiga radi;

BWANA yu juu ya maji mengi.

4 Sauti ya BWANA ina nguvu;

Sauti ya BWANA ina utukufu;

5 Sauti ya BWANA yaivunja mierezi;

Naam, BWANA aivunjavunja mierezi ya Lebanoni;

6 Zab 114:4;Kum 3:9 Airusharusha Lebanoni kama ndama wa ng’ombe;

Lebanoni na Sirioni kama mwananyati.

7 Sauti ya BWANA inatoa miale paa ya moto;

8 Hes 13:26 Sauti ya BWANA yalitetemesha jangwa;

BWANA alitetemesha jangwa la Kadeshi.

9 Sauti ya BWANA yawazalisha ayala,

Na kuiacha misitu wazi;

Na ndani ya hekalu lake

Wanasema, Utukufu!

10 Zab 93:4 BWANA aketi juu ya Gharika;

Naam, BWANA ameshika hatamu ya ufalme milele.

11 Isa 40:29 BWANA na awape watu wake nguvu;

BWANA na awabariki watu wake kwa amani.

Veja também