Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 99

Sifa kwa utukufu wa Mungu

1 Kut 25:22 BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka;

Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.

2 BWANA ni mkuu katika Sayuni,

Naye ametukuka juu ya mataifa yote.

3 Kum 28:58;Isa 6:3;Ufu 4:8 Na walisifu jina lake kuu litishalo;

Ndiye mtakatifu.

4 Kum 32:3,4;Ayu 36:5;Isa 11:3-5;Yer 23:5;Mwa 18:25 Mfalme mkuu99:4 Katika Kiebrania ni nguvu za mfalme. upendaye hukumu kwa haki;

Umeiimarisha haki;

Umefanya hukumu na haki katika Israeli.

5 1 Nya 28:2;Zab 132:7;Isa 66:1 Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;

Sujuduni penye kiti cha miguu yake;

Ndiye mtakatifu.

6 Musa na Haruni walikuwa makuhani wake,

Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake,

Walimlilia BWANA naye akawaitikia;

7 Kut 19:9;33:9;Hes 12:5 Akasema nao katika nguzo ya wingu.

Wakashika shuhuda zake na amri aliyowapa.

8 Hes 14:20;Sef 3:7;Kum 9:20 Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu;

Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe

Ingawa uliwapatiliza matendo yao.

9 Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;

Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu;

Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.

Veja também