Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 15

Mmaa kulawa si ya Kanaani azumiiaye

21 Yesu akahauka hantu hada akaita mwe si ambazo ni hehi na mizi ya Tilo na Sidoni, 22 Aho mvyee yumwe ekuwae ni mkanaani ambae nee kawa akekaa mwe si iyo akamtimia Yesu, nakutoa mgutio, "Zumbe, Mwana wa Daudi, unifiiye mbazi! Mwanangu wa kivyee apishwapishwa ni mazaiko."

23 Iya Yesu khekumwandua mbui yoyose. Aho, wahina wakwe wakambasa Yesu, na kumwamba, "Umwambe aite kwaviya atibasabasa na kutitoeya vuzo!"

24 Yesu akamtambaisa, "Khiagiiwa kwaajii ya wantu wa si ya Isilaeli wakwagao inga ngoto."

25 Iya yuda mmaa akeza na kukinta mavindi hemeso ya Yesu na kumwamba, "Zumbe, niambiize!"

26 Yesu akamtambaisa, "Khio vitana kudoa khande ya wana na kuwatambikia makui."

27 Yuda mmaa akamtambaisa, "Ni kwei Zumbe, akini hata makui yada phuguntio zigwiswazo kulawa he meza za mazumbe wao."

28 Aho Yesu akamtambaisa, "Mmaa uzumizi wako ni mkuu na itende inga wekukundavyo." Yuda mdee akahona kisingi ichoicho.

Veja também