Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 29:7,8

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

7 Kisha makundi ya mataifa yote yanayopigana dhidi ya Arieli,

yale yanayomshambulia yeye na ngome zake,

na kumzingira kwa jeshi,

watakuwa kama ilivyo ndoto,

kama maono wakati wa usiku:

8 kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula,

lakini huamka, bado njaa yake ingalipo,

kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji,

lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu.

Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa

yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    7 Na wingi wa mataifa wapiganao na Arieli, wote wapiganao naye na ngome yake, na wanaomwudhi, watakuwa kama ndoto, na maono ya usiku. 8 Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe, anakula; lakini aamkapo, nafsi yake haina kitu; na kama mtu mwenye kiu aotapo, kumbe, anakunywa; lakini aamkapo, kumbe, anazimia, na nafsi yake inatamani; hivyo ndivyo utakavyokuwa huo wingi wa mataifa waletao vita juu ya mlima Sayuni.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    7 Kisha makundi ya mataifa yote yale yapiganayo dhidi ya Arieli,

    yale yanayomshambulia yeye na ngome zake, na kumzunguka kwa jeshi,

    watakuwa kama ilivyo ndoto,

    kama maono wakati wa usiku:

    8 kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula,

    lakini huamka, bado njaa yake ingalipo,

    kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji,

    lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu.

    Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa

    yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.