Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 43:1,2,18,19

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Mwokozi pekee wa Israeli

1 Lakini sasa hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu,

yeye aliyekuumba, ee Yakobo,

yeye aliyekuhuluku, ee Israeli:

"Usiogope kwa maana nimekukomboa,

nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu.

2 Unapopita kwenye maji makuu,

nitakuwa pamoja nawe,

unapopita katika mito ya maji,

hayatakugharikisha.

Utakapopita katika moto,

hutaungua,

miali ya moto haitakuunguza.

18 "Msiyakumbuke mambo yaliyopita,

wala msiyatafakari mambo ya zamani.

19 Tazama, nitafanya jambo jipya!

Sasa litachipuka, je, hamtalitambua?

Nitafanya njia jangwani

na vijito vya maji katika nchi kame.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Isa 44:6;42:6;1 Kor 1:9;2 Tim 1:9Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. 2 Zab 66:12;Kum 31:6-8;Dan 3:25Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.

    18 Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. 19 2 Kor 5:17;Ufu 21:5Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Lakini sasa hili ndilo asemalo Bwana,

    yeye aliyekuumba, ee Yakobo,

    yeye aliyekuhuluku, ee Israeli:

    "Usiogope kwa maana nimekukomboa,

    nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu.

    2 Unapopita kwenye maji makuu,

    nitakuwa pamoja nawe,

    unapopita katika mito ya maji,

    hayatakugharikisha.

    Utakapopita katika moto,

    hutaungua,

    miali ya moto haitakuunguza.

    18 "Msiyakumbuke mambo yaliyopita,

    wala msiyatafakari mambo ya zamani.

    19 Tazama, nitafanya jambo jipya!

    Sasa litachipuka, je, hamtalitambua?

    Nitafanya njia jangwani

    na vijito vya maji katika nchi kame.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.