3 "Nisikilizeni mimi, ee nyumba ya Yakobo,
ninyi nyote mliobaki wa nyumba ya Israeli,
ninyi ambao nimewategemeza tangu mlipotungwa mimba,
nami nimewabeba tangu kuzaliwa kwenu.
4 Hata wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye,
Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.
Nimewahuluku, nami nitawabeba,
nitawahudumia ninyi na kuwaokoa.