13 Pigeni kelele kwa furaha, enyi mbingu;
furahi, ee dunia;
pazeni sauti kwa kuimba, enyi milima!
Kwa maana Mwenyezi Mungu anawafariji watu wake,
naye atakuwa na huruma kwa watu wake walioumizwa.
14 Lakini Sayuni alisema, "Mwenyezi Mungu ameniacha,
Bwana amenisahau."
15 "Je, mama aweza kumsahau mtoto
aliye matitini mwake akinyonya,
wala asiwe na huruma
juu ya mtoto aliyemzaa?
Ingawa anaweza kusahau,
mimi sitakusahau wewe!
16 Tazama, nimekuchora kama muhuri
katika vitanga vya mikono yangu,
kuta zako zi mbele yangu daima.