Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaya 49:14-16

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

14 Lakini Sayuni alisema, "Mwenyezi Mungu ameniacha,

Bwana amenisahau."

15 "Je, mama aweza kumsahau mtoto

aliye matitini mwake akinyonya,

wala asiwe na huruma

juu ya mtoto aliyemzaa?

Ingawa anaweza kusahau,

mimi sitakusahau wewe!

16 Tazama, nimekuchora kama muhuri

katika vitanga vya mikono yangu,

kuta zako zi mbele yangu daima.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    14 Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. 15 Zab 103:13;Mt 7:11;Rum 11:29Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. 16 Kut 13:9;Wim 8:6;Zek 2:8Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    14 Lakini Sayuni alisema, "Bwana ameniacha,

    Bwana amenisahau."

    15 "Je, mama aweza kumsahau mtoto

    aliyeko matitini mwake akinyonya,

    wala asiwe na huruma

    juu ya mtoto aliyemzaa?

    Ingawa anaweza kusahau,

    mimi sitakusahau wewe!

    16 Tazama, nimekuchora kama muhuri

    katika vitanga vya mikono yangu,

    kuta zako zi mbele yangu daima.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.