3 Alidharauliwa na kukataliwa na wanadamu,
mtu wa huzuni nyingi, ajuaye mateso.
Kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao,
alidharauliwa, wala hatukumhesabu kuwa kitu.
4 Hakika alichukua udhaifu wetu
na akajitwika huzuni zetu;
tulidhania kuwa ameadhibiwa na Mungu,
naye akapigwa sana na kujeruhiwa.
5 Lakini alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu,
alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu;
adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake,
na kwa majeraha yake sisi tumepona.