Utukufu wa baadaye wa Sayuni
1 "Imba, ewe mwanamke tasa,
wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto;
paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha,
wewe ambaye kamwe hukupata uchungu;
kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi
kuliko wa mwanamke mwenye mume,"
asema Mwenyezi Mungu.