Utukufu wa Sayuni
1 "Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja
na utukufu wa Mwenyezi Mungu umezuka juu yako.
2 Tazama, giza litaifunika dunia,
na giza nene litayafunika mataifa,
lakini Mwenyezi Mungu atazuka juu yako
na utukufu wake utaonekana juu yako.
3 Mataifa watakuja kwenye nuru yako
na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.