Pular para o conteúdo
Publicidade

Isaías 9

6 Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,

tumepewa mtoto wa kiume,

nao utawala utakuwa begani mwake.

Naye ataitwa

Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,

Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

7 Kuongezeka kwa utawala wake na amani

hakutakuwa na mwisho.

Atatawala kwenye kiti cha utawala cha Daudi

na juu ya ufalme wake,

akiuthibitisha na kuutegemeza

kwa haki na kwa adili,

tangu wakati huo na hata milele.

Wivu wa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni

utatimiza haya.

Veja também