KITABU CHA PILI
1 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye;
Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.
2 Zab 49:6;Lk 12:19;Dan 4:27 Hazina za uovu hazifaidii kitu;
Bali haki huokoa na mauti.
3 Zab 10:14 BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa;
Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
4 Mit 13:4 Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini;
Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha.
5 Akusanyaye wakati wa joto ni mwana mwenye hekima;
Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
6 Est 7:8 Baraka humkalia mwenye haki kichwani;
Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu.
7 Zab 9:5,6;Mhu 8:10 Kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka;
Bali jina la mtu mwovu litaoza.
8 Aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo;
Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.
9 Zab 23:4;Isa 33:15,16 Aendaye kwa unyofu huenda salama;
Bali apotoshaye njia zake atajulikana.
10 Akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko;
Bali mpumbavu mwenye maneno mengi ataanguka.
11 Zab 37:30;107:42 Kinywa chake mwenye haki ni chemchemi ya uzima;
Bali jeuri hufunika kinywa chake mtu mwovu,
12 Yak 5:20;1 Pet 4:8;1 Kor 13:4 Kuchukiana huleta fitina;
Bali kupendana husitiri makosa yote.
13 Lk 4:22 Hekima hupatikana midomoni mwa mwenye ufahamu;
Bali fimbo hufaa kwa mgongo wake asiye na ufahamu.
14 Watu wenye akili huweka akiba ya maarifa;
Bali kinywa cha mpumbavu ni uangamivu ulio karibu.
15 Ayu 31:24;Mit 18:11;Lk 12:19;1 Tim 6:17 Mali ya tajiri ndio ngome yake;
Ufukara wa maskini ndio umwangamizao.
16 Kazi yake mwenye haki huuelekea uzima;
Mazao ya wabaya huielekea dhambi.
17 Akubaliye kurudiwa huwa katika njia ya uzima;
Bali yeye aachaye maonyo hukosa.
18 Yeye afichaye chuki ana midomo ya uongo,
Na yeye asingiziaye ni mpumbavu.
19 Mhu 5:3;Zab 39:1;Mit 17:27,28;Yak 1:19 Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu;
Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili.
20 Ulimi wa mwenye haki ni kama fedha safi;
Moyo wa mtu mbaya haufai kitu.
21 Midomo ya mwenye haki hulisha watu wengi;
Bali wapumbavu hufa kwa kuwa hawana ufahamu.
22 Mwa 12:2;Kum 8:17,18;1 Sam 2:7,8;1 Tim 4:8 Baraka ya BWANA hutajirisha,
Wala hachanganyi huzuni nayo.
23 Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo;
Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima.
24 Ayu 15:21;Mt 5:6 Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia;
Na wenye haki watapewa matakwa yao.
25 Zab 15:5;Mt 7:24;1 Tim 6:19 Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena;
Bali mwenye haki ni msingi wa milele.
26 Kama siki menoni, na kama moshi machoni,
Ndivyo alivyo mtu mvivu kwa hao waliomwajiri.
27 Mhu 7:17 Kumcha BWANA kwaongeza siku za mtu;
Bali miaka yao wasio haki itapunguzwa.
28 Zab 16:9;Rum 5:2;Ayu 8:13 Matumaini yao wenye haki yatakuwa furaha;
Bali matarajio yao wasio haki yatapotea.
29 Zek 10:12;Flp 4:13;Isa 40:31;Zab 1:6 Njia ya BWANA ni kimbilio lake mtu mkamilifu;
Bali ni uharibifu kwao watendao maovu.
30 Mwenye haki hataondolewa milele;
Bali wasio haki hawatakaa katika nchi.
31 Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima;
Bali ulimi wa ukaidi utakatiliwa mbali.
32 Midomo ya mwenye haki huyajua yatakayokubaliwa;
Bali kinywa chao wasio haki hunena ukaidi.