Pular para o conteúdo
Publicidade

Mithali 16:1-3,9,25,33

SRUV Swahili Revised Union Version

1 Mt 10:19Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu;

Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.

2 1 Sam 16:7;Dan 5:27Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;

Bali BWANA huzipima roho za watu.

3 Mkabidhi BWANA kazi zako,

Na mawazo yako yatakuwa kweli.

9 Yer 10:23Moyo wa mtu huifikiri njia yake;

Bali BWANA huziongoza hatua zake.

25 Mit 14:12Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu;

Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

33 Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo;

Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,

    bali jibu la ulimi hutoka kwa Mwenyezi Mungu.

    2 Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe,

    bali makusudi hupimwa na Mwenyezi Mungu.

    3 Mkabidhi Mwenyezi Mungu lolote ufanyalo,

    nayo mipango yako itafanikiwa.

    9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake,

    bali Mwenyezi Mungu huelekeza hatua zake.

    25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,

    bali mwisho wake huelekeza mautini.

    33 Kura hupigwa kwa siri,

    lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Mwenyezi Mungu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,

    bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.

    2 Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe,

    bali makusudi hupimwa na Bwana.

    3 Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo,

    nayo mipango yako itafanikiwa.

    9 Moyo wa mtu huifikiri njia yake,

    bali Bwana huelekeza hatua zake.

    25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,

    bali mwisho wake huelekeza mautini.

    33 Kura hupigwa kwa siri,

    lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.