1 Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe;
Hushindana na kila shauri jema.
2 Mpumbavu hapendezwi na ufahamu;
Ila moyo wake udhihirike tu.
3 Ajapo asiye haki, huja dharau pia;
Na pamoja na aibu huja lawama.
4 Zab 78:2 Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi;
Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.
5 Law 19:15;Kum 1:17;Ayu 13:7,8;Mit 24:23 Kukubali uso wake asiye haki si vizuri;
Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.
6 Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina,
Na kinywa chake huita mapigo.
7 Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake,
Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.
8 Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo;
Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.
9 Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake,
Ni ndugu yake aliye mharibifu.
10 2 Sam 22:3,51;Zab 18:2 Jina la BWANA ni ngome imara;
Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.
11 Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;
Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.
12 Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna;
Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.
13 Yeye ajibuye kabla hajasikia,
Ni upumbavu na aibu kwake.
14 Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake;
Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?
15 Efe 1:17 Moyo wa mwenye busara hupata maarifa;
Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.
16 Mwa 39:2-6;41:14,38-44;Dan 1:17-20;6:3 Zawadi ya mtu humpatia nafasi;
Humleta mbele ya watu wakuu.
17 Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki;
Lakini jirani yake huja na kumchunguza.
18 Kura hukomesha mashindano;
Hukata maneno ya wakuu.
19 Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu;
Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.
20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake;
Atashiba mazao ya midomo yake.
21 Mt 12:37 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi;
Na wao waupendao watakula matunda yake.
22 Apataye mke apata kitu chema;
Naye ajipatia kibali kwa BWANA.
23 Mwa 42:13-16;Yak 2:3 Maskini hutumia maombi;
Bali tajiri hujibu kwa ukali.
24 Yn 15:14,15 Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe;
Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.