Thamani ya hekima
1 Mwanangu, kama ukiyakubali maneno yangu,
Na kuyaweka akiba maagizo yangu;
2 Hata ukatega sikio lako kusikia hekima,
Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu;
3 Naam, ukiita busara,
Na kupaza sauti yako upate ufahamu;
4 Zab 19:10;Mit 3:14,15;Mt 6:19-21Ukiutafuta kama fedha,
Na kuutafutia kama hazina iliyositirika;
5 Ndipo utakapofahamu kumcha BWANA,
Na kupata kumjua Mungu.
6 Lk 21:15;Yn 6:45;Yak 1:5Kwa kuwa BWANA huwapa watu hekima;
Kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu;