Wimbo kwa mke Mwema
10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana thamani yake yapita thamani ya marijani.
11 Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato.
12 Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake.
13 Hutafuta sufu na kitani;
Hufanya kazi yake kwa moyo wote.
14 Afanana na merikebu za biashara;
Huleta chakula chake kutoka mbali.
15 Rum 12:11;Mt 24:45;Lk 12:42Tena huamka, kabla usiku haujaisha;
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;
Na wajakazi wake sehemu zao.
16 Huangalia shamba, akalinunua;
Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;
Hutia mikono yake nguvu.
18 Huona kama bidhaa yake ina faida;
Taa yake haizimiki usiku.
19 Hutia mikono yake katika kusokota;
Na mikono yake huishika pia.
20 Huwakunjulia maskini mikono yake;
Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.