Ushauri wa mzazi
1 Zab 34:11;Mit 1:8Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu,
Tegeni masikio mpate kujua ufahamu.
2 Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri;
Msiiache sheria yangu.
3 2 Sam 12:24;1 Nya 29:1Maana nilikuwa mwana kwa baba yangu,
Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu.
4 1 Nya 28:9;Efe 6:4Naye akanifundisha, akaniambia,
Moyo wako uyahifadhi maneno yangu;
Shika amri zangu ukaishi.
5 Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau;
Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu.
6 2 The 2:10Usimwache, naye atakusitiri;
Umpende, naye atakulinda.